Sikumbuki mara ya mwisho nikiandika chochote kwa hii lugha. Nafikiri ilikuwa katika mtihani wa fasihi ya KCSE. Lahaula! Nimesahau vitu kama minyambuliko wa vitenzi, mithali na kadhalika. Ninashuku kama ninaweza kufunza mtu yoyote kuhusu kiswahili. Nifanyeje? Labda nitaanza kuandika hapa saa zingine kwa lugha halafu tuone itaendeleaje? Labda hata siku nyingine hivi karibuni, nitaandika hapa kuhusu "Jifunze kiswahili". Au sio?